Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Thursday, February 26, 2015

ALLAN KINGDOM: RAPPER MTANZANIA ALIYESHIRIKISHWA NA KANYE WEST KWENYE NGOMA MPYA 'ALL DAY'(DETAILS)

Kanye west anafahamika kwa kuwatoa wasanii wangu wakubwa nchini Marekani.Bila yeye leo hii hakuna mtu angekuwa anawajua Big Sean na John Legend. Na sasa kupitia ngoma yake mpya 'all day' (ambayo hakuna shaka itakuwemo kwenye album yake mpya),yeezy anamweka kwenye ramani ya muziki duniani,rapper Mtanzania aishie Minnesota,Marekani Allan Kingdom.

Hakuna mkazi wa Minnesota asiyemjua rapper huyu na infact ni superstar tayari pande hizo japo tunasikitika kuwa tumemfahamu sasa kupitia Kanye West aliyemshirikisha kwenye ngoma yake ambayo tayari inapendwa na ilivuja wiki iliyopita.

Kinachotufurahisha zaidi ni kuwa Kanye amempandisha rapper huyo jana (jumatano)kwenye Brit Awards (zenye level sawa na tuzo za Grammy za Marekani)zilizofanyika jijini London kutumbuiza ngoma hiyo.

Kwa mujibu wa Star Tribune,Kanye atakuwa amemfahamu Allan kupitia mkurugenzi wake wa ubunifu, Virgil Abloh ambaye ni sehemu ya watu walio kwenye kambi ya Allan. Hakitakiwa kitu cha ajabu kama akishawishika pia kumeongeza kwenye list ya wasanii wa lebo yake,GOOD MUSIC.

ALLAN KINGDOM NI NANI?
Mwaka jana mtandao wa komplex ulimjumuisha kwenye orodha ya rappers 25 wapya wa kuwaangalia mwaka 2014. Allan Kingdom ni rapper na producer wa musiki mwenye makazi yake St paul ,Minnesota nchini Marekani.

Alizaliwa kwa jina la Allan Kyaringa miaka 21 iliyopita nchini Kanada na mama yake kutoka Tanzania na baba kutoka Afrika kusini.

"Naweza kuzoea kiurahisi kabisa kwenye mazingira tofautitofaiti, lakini sijawahi kuhisi kiukweli kuwa Mimi ni sehemu ya jamii moja". Rapper huyo aliliambia gazeti kubwa zaidi la kila siku katika jumbo la Minnesota,Star tribune.

Mtindo wake wa muziki unachukua sana vionjo pia kutoka Afrika Mashariki kupitia muziki ambao mama yake alikuwa akiskiliza alipokuwa mdogo na kuchanganya na ladha za waimbaji wanaomuenspire kama Frank Ocean Odd Future,Earl Sweatshirt na Kid Cudi.

Uhusiano wake na Kidd Cud ni mkubwa zaidi kwa kuwa mmoja wa watayarishaji wa Cud,Plain Pat ni meneja wa Allan.

"Aliniambia nimetishwa sana na production yako,"Pat anamkumbushia Allani ambaye kipindi hicho alikuwa na miaka 17 kupitia Twitter.

Akiwa mtoto wa pekee wa wazazi wake,ametumia mda mchache mno kukaa na baba mtoto aliyerudi Afrika kusini wakati Allan akiwa mtoto. Kwa hiyo amelelewa zaidi na mama yake Mtanzania.

Wazazi wake walikutana wakati skiwa wanasomo kwenye chuo kikuu cha Manitoba, huko winnipeg nchini Canada na aliishi huko hadi darasa la 3.
Mama yake Laurentian aliwahi kumleta Tanzania mara kadhaa na kumfundisha utamaduni wa nyumbani.

Akiwataja wasanii wakongo kama vile Koffi olomide,Papa wemba,Allan alisema
  "Mwanzoni nilipoanza kutoa nyimbo watu walisema walikuwa wakisikia hiyo 'influence' na kwakweli kilikuwa ni kitu kinachotokea bila kujua (subconscious). Lakini nilifikiria,'ok, basi naweza kuimiliki pia. Na ndipo nikaanza kusikiliza nyimbo hizo Mimi mwenyewe."

Ushawishi kutoka kwa mtengenezaji wa nyimbo za Kanye unasikika kwenye EP yake ya miaka miwili iliyopita,trucker music iliyodhihirisha kipaji kilichopevuka katika umri wake mdogo.

Akiongea na Papermag.com mwaka jana,Allan alisema  Minnesota ni sehemu yenye wahamiaji wengi wakigeni kutoka Afrika Mashariki na hivyo kumfanya kujisikia yupo nyumbani.

"Ninaweza kusimama sehemu na kupata kitu kinacho fanana na kile mama yangu angetengeneza,"alisema.

Kazi yake mpya inaitwa Future Memories yenye jumla nyimbo 12  zikiwemo Wavey na  Evergreen.

No comments:

Post a Comment