Mlinzi wa timu ya Liverpool,Kolo Toure amethibitisha Kuwait amestaafu kuchezea soka la kimataifa baada ya kuwa na kikosi. Cha timu ya taifa Ivory Coast kwa mda wa miaka 15,ambapo ameshiriki pia amesaidia kuisaidia timu ya hiyo kutwaa kombe LA mataifa ya Afrikaans Afcon2015
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ,aliweka wazi Kuwa mchezo wake wa mwisho kuonekana kwenye dimba LA soka LA kimataifa ulikuwa dhidi ya timu ya Equatorial Guinea.
Kolo anasema anaipenda nchi yake na hasa anachokipenda zaidi maishani mwake ni mchezo wa soka,lakini amesisitiza huu ni wakati wake muafaka kustaafu soka la kimataifa.
"Najisikia vibaya sana kuwafahamisha kuwa ni wakati wangu kuwaaga,lengo langu lilikuwa kushinda katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika,nakubali ulikuwa ni uamuzi mgumu kufanya"-Kolo
No comments:
Post a Comment