Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Friday, February 27, 2015

KIJANA AKANA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI WA MIAKA 16

Mkazi wa Tabata,Erasto Clement (22) amepandiswa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na kukana mashitaka ya kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato ya kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenyewe  umri wa miaka 16.

Akisomewa  maelezo ya awali jana, wakili wa serikali Fosta Mosha alidai mbele ya Hakimy Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan Kuwa katika tarehe na mwezi usiofahamika,mwaka jana,Clement pamoja na mlalamikaji walidaiwa kuwa wanafamiana kwa muda mrefu.

Mosha alidai kuwa septemba,2013 mshitakiwa na mlalamikaji waliamza mahusiano ya kimapenzi na kumuingilia kimwili mlalamikaji huyo huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Pia alieleza kuwa mlalamikaji  aliripoti taarifa hizo kituo cha polisi na kupewa  PF3 kwa ajili ya kwenda hospitali.

Wakili Misha alidai kuwa mlalamikaji alipofika hospitali alipimwa na kukutwa na ujauzito wa  miezi 6.

Mshitakiwa alikubali maelezo binafsi pia alikana kufikishwa mahakamani hapo kusomewa mashitaka yanayomkabili.

Hata hivyo,upande wa jamhuri ulidai kuwa utakuwa na mashahidi manne na kielezo kimoja ambacho ni PF3.

Hakimu Hassan aliahirisha kesi hiyo had I April mosi mwaka huu itakapoanza kusikilizwa.

No comments:

Post a Comment