Kobe wadogo 250, wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Aman Karume,wakiwa njiani kusafirishwa kwa njia ya magendo kwenda Malaysia.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mk Adam Khamis Mk Adam,alisema kobe hao walikamatwa wakiwa wamehifadhiwa katika masaduku yaliyowekwa maembe ndani yake,katika hatua za mwisho za kusafirishwa.
"Ni kweli tumekamata Kobe 250 wakiwa wamehifsdhiwa vizuri katika masanduku yakiwa yameingizwa maembe tayari kusafirishwa kwenda Malaysia" alisema.
Hata hivyo Kamanda Hamdani alikataaa kumtaja mtu aliyekamatwa na kobe halo kwa madai kwamba uchunguzi unaendelea na kitendo cha kumtaja moja moja,kinawez kuharibu uchunguzi wa tukio hilo.
"Jeshi la Polisi kwa sasa halipo tayari kumtaja mtuhumiwa aliyekamatwa na Kobe hao kwa sababu za uchunguzi zaidu unaendelea....unajuwa ukianza kuntaja mtuhuniwa pamoja na wangu wengine,unaharibu uchunguzi mzima wa tukio hilo" Alisema.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na matukio ya wizi wa Kobe kutoka Zanzibar kupelekwa sehemu nyingine duniani ikiwa ni pamoja na Tanzania Bara.
Kobe hao wanalindwa na sheria za Kimataifa,wakiwa katika orodha ya viumbe ambao wapo katika hatari ya kutoweka duniani,kama ilivyo kwa sasa kwa hivyo wamekuwa katika udhibiti mkubwa.
Kwa upande wa Zanzibar,Kobe wanahifadhiwa katika kisiwa kidogo cha Chum be kilichopp nje ya Bandari ya Malindi umbali wa kilomita 40,ambapo hata hi yo kumekuwepo matukio ya wizi wa mara kwa mara.
Ofisa mmoja kutoka Kamisheni ya Utalii Zanzibar, ambaye moja ya majukumu yake ni kulinda na kuhifadhi Kobe waliopo katika kisiwa kidogo cha changu,alikiri kuwepo wizi katika nyakati tofauti,unaofanywa na watu wasiokuwa waaminifu wanaotembelea kisiwa hicho cha shuguli za utalii.
"Yapo matukio ya Wizi wa Kobe katika kisiwa cha changu kwa nyakati tofauti,kwani watu hufika katika kisiwa kwa shughuli tofauti ikiwemo za matembezi"alisema.
Katika miaka kumi iliyopita,zaidi ya Kobe 1,500 wameibiea katika kisiwa cha changuu,wakiwemo Kobe wadogo wanao hifadhiwa sehemu maalumu.
No comments:
Post a Comment