Mkazi wa kijiji cha Ibosa ,Kata ya Nyakato,Wilaya ya Bukoba Vijijini,Amelia Richard(50) anatuhumiwa Kumua mwanamke mwenzake kwa kumwagia mafuta ya taa na kumchoma moto baada ya kumfumania na mumewe.
Kamanda wa Polisi wa mkoa Kagera,Henry Mwaibabe alitaja tukio hilo ni la Februari 15,mwaka huu saa 3 usiku katika kijiji cha Ibosa Kara ya Nyakata Bukoba vijijini.
Alimtaja aliyeuwa ni Pelagia Martin(46) aliyeunguzwa mwili mzima.Kamanda alisema mwanamke huyo alichelewesha kufikishwa Hospitali ya Mkoa hadi kesho yake,February 16 baada ya wanafamilia kuomba wayamalize bila kwenda Polisi.
Makubaliano ya wanafamilia halo yalitokana na kile kinachonekana kwamva Amelia alimfumania Pelagia akiwa na mumewe,Richard Bulebo (57) ndani ya nyumba yao.
Kwa mujibu wa Kamanda,February 16 walipoona hali ya majeruhi inazidi kuwa mbaya,ndipo walifika katika kituo cha Polisi mjini kati wakiomba msaada.
Polisi walimpeleka majeruhi huyo Hospitali ya mkoa lakini alifariki kabla ya kupatiwa matibabu.Polisi inawashikilia Amelia name Bulebo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment