Kufuatiwa kifo cha ghafla kapteni mstaafu wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) na mbunge wa mbinga magharibi mkoani Ruvuma kupitia leseni ya CCM John Damian Mtokambali Komna (61),staa wa sinema za kibongo Elizabeth Michael (Lulu) anadaiwa kuathirika kisaikolojia kutokana na kushambuuliwa kwa matusi mitandaoni.
Baada ya Komba kufariki dunia jumamosi iliyopita baadhi ya watanzania wasio na soni walianza kumtumia salamu za pole Lulu kwa madai kwamba aliwahi kuhutumiwa kutoka na mheshimiwa huyo.
"Eti mwanaume kama una jina linaloishia na 'mba' kama komba au kanumba (marehemu Steven Kanumba) basi imekula kwake", kilisema chanzo hicho na kufafanua Kuwa maneno hayo yameuchoma moyo wake kwa kiasi kwamba anahitaji ushauri wa kisaikilojia.
Ilisemekana kwamba hali hiyo imemkosesga raha na kuwaona baadhi ya watanzania ni watu wasiojua maumivu ya moto,kwani ana moyo wa nyama na si wa Chuma.
Chanzo kinasema, kilieleza kuwa umri wa lulu wa miaka 20 amebebeshwa mzigo mzito mno hadi ya kufikia hatua ya kutamka waziwazi "watanzania imetosha nimewakosea nini? Naombeni mnihurumie jamani"
Kwa mujibu wa chanzo hicho pamoja na kwamba lulu anafanya vizuri kwenye masomo yake katika chuo cha utumishi wa umma (TPSC),kilichopo Magogoni Posts jijini Dar es Salaam,kuna kila dalili akashindwa kufunika kawaida yake kutokana kuwa na msongo.
"Unajua wakati mwingne anaogopa hata kuingia kwenye mitandao ya kijamii kama whatsapp na instagram kwa sababu huko ndiko kuna sarakasi na matusi yasiyokuwa na kichwa wala miguu."
"Muda mwingi ana kuwa hana raha. Anawaza sana hata sisi wenyewe inabidi kumlinda ili asichukue uamuzi wowote mbaya kwa sababu kiukweli hayuko vizuri kisaikolojia hata yeye mwenyewe anakiri hilo kuwa kinamuathiri mno kwenye maisha yake." Kilisema chanzo hicho kilichomba kisitajwe jina.
Baada ya kunyetishwa kuhusu ukubwa wa ishu hiyo na namna lulu anavyoteseka ,Gazeti la Ijumaa lilimtafuta staa huyo kwa bahati mbaya hawakumpata kwa sababu alikuwa darasani. Na ndipo tukamtafuta mama yake mzazi Lucresia Karugila. Na kusema haya
"Nashangaa watu wangu wanavyomuandama name kumtafuta mwanangu"
"Kiukweli inasikitisha sana tena sana,sijui mwanangu amewakosea nini? Wakati wa kifo cha Kanumba ( April 7 2012) watu walusema mtu wa mwisho kuwasiliana na lulu ni Komba,lakini baada ya uchunguzi wa polisi ikagundulika mtu wa mwisho kuwasiliana nae alikuwa binamu yake jaila," aliongezea mama lulu.
Baada ya kuzungumza na mama mzazi wa Lulu, Ijumaa ilimtafuta tena lulu na kufanikiwa kumpata. Lulu alishangazwa sana taarifa za uwongo zinazoenezwa na watanzania.
"Awali nilikuwa sielewi nikawa nashangaa napewa pole,nikauliza pole za nini?"
"Kiukweli watanzania wanashangaza sana wanapenda sana kuzungumza mambo ambayo hawana uhakika nayo."
"Badala wanishauri mambo ya kazi,wanaeneza mambo yasiyo na kichwa wala mguu"
"Naombeni watanzania wajue kuwa na mimi ni binadamu,wanihurumie." Alisema lulu.
Chanzo cha habari: Gazeti la Ijumaa/GPL
No comments:
Post a Comment