Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Monday, February 23, 2015

JELA MAISHA KWA KUMBAKA MTOTO MIAKA MITANO NA KUMWAMBUKIZA UKIMWI.

Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Nzega mkoani Tabora imemhukunu kifungo cha maisha Kashindije Shija (50), baada ya kupatikana na kosa la kumbaka  mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

Akisoma hukumu hiyo mwishoni mwa wiki,Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Nzega Joseph Ngomero,alisema kuwa,kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo,amelazimika kutoa hukumu hiyo ili iwe fundishi kwa watu wengine wanaokusudia kufanya vitendo kama hivyo.

Hakimu Ngomero aliongeza kwa kusema kuwa,kutokana na kitendo cha kinyama alichokufanya Shija cha kum aka motto mwenye umri wa miaka 5,mahakama hiyo imelazimika kumhukumu kifungi cha maisha jela.

Awali Mwendesha Mashitaka wa Seriali wilayani Nzega Melito Ukongoji aliiambia mahakama hiyo kuwa,mnamo Mei 19,2014 katika kijiji cha Kidete wilayani Nyega saa 8 mchana,Shija  alifumaniwa chini ya mti wa mwembe akiwa anambaka mtoto huyo.

Aisha Melito aliongeza Kuwait kutokana na kitendo alichokifanya mtuhumiwa kilimsababisha mtoto huyo maumivu makali katika mwili wake pamoja na kutoka damu nyingi.

Mwendesha mashitaka huyo,aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu Kali,iwe fundisho kwa watu wengine we ye tabia kama hizo.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa,Mahakama hiyo ilitoa nafasi ya utetezi kwa mtuhumiwa ambapo aliiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu kutokana na kutokana na kuwa mwathirika wa virusi vya Ukimwi.

No comments:

Post a Comment