Meneja wa zamani wa Diamond Platinumz,Msafiri Misifa maarufu kama Papa Misifa amesema wasanii wengi wanashindwa kuendelea kutokana na kushindwa kuhifadhi wanachokipata.
Papa Misifa aliyewahi pia kuwa meneja wa Dully Skyes na Cassim Mganga,ameiambia WAKEREKETWA kuwa Diamond ni msanii pekee aliyeweza kufata mafunzo yake na ndo maana anaendelea kufanikiwa mpaka sasa.
"Tatizo kubwa sana la wasanii wanapopata riziki wanashindwa kujipangalia. Na mafunzo mengi niliyompa diamond ndo maana mpaka leo anajua kujipangalia mpaka pale alipofika. Wasanii wanashindwa kupangilia pesa zao,tatizo wanapopata pesa wanabadilika. Ukitaka kujua tabia ya mwanadamu ngoja apate pesa ndo utajua tabia yake"amesisitiza..
" wasanii wengi hawalengi kufanya vitu vya maendeleo,wanalenga kufanya starehe kwenye baa. Ndo maana watu wanasema wanamziki wa zamani wamefulia,ni kweli kwasababu hawakujipanga. Hawakutambua kesho yao,wewe unafikiri kwa nini Diamond anaiogopa kesho yake? Ni kutokana na maisha yalivyo,ukipata nafasi itumie ipasavyo."
No comments:
Post a Comment