Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Monday, February 16, 2015

ELIMU YA TANZANIA SASA KUENDESHWA KISIASA.NA UBORA WAKE UTAZIDI KUENDELEA KUPOROMOKA

Wiki iliyopita raisi wetu wa Tanzania,Prof.Jakaya Kikwete,alifuta ada kwa elimu ya sekondari,na  mtihani wa darasa la saba,kwa lengo la elimu ya kidato cha nne kuwa ya lazima kwa kila mtu kuwa nayo.Kufutwa kwa mitihani ya darasa la saba,itampelekea mwanafunzi kusoma miaka 11 bila kufanya mitihani ya taifa,kwa hii itapelekea wanafunzi kubweteka kujifunza,na kuongezeka kwa wimbi la wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika.
Hivi majuzi matokeo ya wanafunzi ya kidato cha nne (2014) yalitoka huku takwimu zikionesha ongezeko limeongezeka kwa asilimia 10.Ila matokeo hayo yamejaa uozo mtupu na udanganyifu kwa umma,kwani matokeo yametolewa kwa mfumo wq GPA,ambazo watahiniwa  au wahitimu hawawezi kuzichanganua ili kujua GPA husika inamaanisha nini? ,na wameenda mbali zaidi kutoa GPA zisizofanana hata kidogo na zile za vyuo,ili hata ndugu wa wahitimu hao wasiweze kuzichanganua.Walisema madaraja yatakuwa hivi:-
    0.0-0.1   FAIL
    0.2-1.5   PASS
    1.6-2.5   CREDIT
    2.6-3.5   MERIT
    3.6-5      DISTINCTION
Kutokana na zile pass ambazo mtu anakuwa amepata kwenye somo husika ,kwa kufuata mtiririko huu ufuatao:-
     A=75-100
     B+=60-74
     B=50-59
     C=40-49
     D=30-39
     E=20-29
     F=0-19
Kwa maana hiyo ukipata marks kulingana na grade hizo utakuwa unaangukia kwenye mojawapo ya alama hi I
     A=5
     B+=4
     B=3
     C=2
     D=1
     E=0.5
     F=0
Lakini tatizo bado lipo kwa wale wa wataalamu wa kukotoa ,wakijaribu kutumia alama hizo,kukokotoa matokeo ya mtu wanakuta alichaandikiwa kama ni  pass au distinction hakifanani na ukokotozi sahihi ,kwa mfano mtu aliyepata
     Civics-C
     History-C
     Geography-C
     Kiswahili-B
     English-B
     Physics-B
     Chemistry-B
     Biology-B
     Maths-D
Ukikokotoa kulingana na mfumo wao na grade zao zilivyopangwa unapata 2.44 ambayo ni CREDIT,ila wao wanamuandikia 2.7 ambayo ni MERIT.Kuna tatizo hapa,watanzania  tumekuwa wajinga sana huwezi kumpa mtu matokeo ambayo ata yeye hayaelewi.ELIMU NI BURE.

No comments:

Post a Comment