Watu watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto kuteketea kabisa akiwemo dereva na utingo wale baada ya Lori la mafuta kuacha njia na kupinduka na kuungua moto katika eneo LA Maseyu Barbara ya Morogoro Dar es Salaam.
Mwandishi wetu alishuhudia kikosi cha zimamoto ambao wakichukua muda kuuzima huo moto kutokana na kusambaa ambapo hata hi yo hakukua na matukio ya wangu kujitojeza kuiba mafuta kama ilivyozoeleka.
Baada ya kumaliza kuuzima moto huo kikosi cha zimamoto na uokoaji wakafanya juhudi nyingine za kuvuta kwa craine na kukata kwa kutumia mashoka mabaki ya Lori hilo baada ya walioshuhudia tukio. Kueleza kuwa gari hawakutoka ambapo baada ya muda miili mitatu iliokolewa ikiwa imeungua kabisa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo madereva wa malori ambapo walukuwa wakisafirisha mafuta katika kampuni moja Farhan Yusuf amesema Lori hilo lilikuwa lumesheheni mafuta ya Dezel mali ya kampuni ya Petrol Africa ilikuea ikitokea Dar es salaam kwenda jijini Mwanza ambapo ilipoteza muelekeo na kupinduka Kisha kuwaka moto.
Waliofariki dunia ni Ahmed Dilie dereva na utingo wake aliyefahamika kwa majina ya Emela na mtu mmoja ambaye hakuweza fahamika mara moja.
Nao wananchi walioshuhudia tukio hill wameeleza jinsi tukio lilivyotokea ambapo wananchi wanelalamika eneo hilo kuwa limekuwa na matukio mengi ya ajali na hivyo kuomba serikali kuona umuhimu kuweka vituo vya zima moto katika eneo hilo kwani magari ya zimamoto yalichukua muda mrefu kufika kwenye eneo la tukio kutokana na umbali mrefu.
Nae Afisa mkaguzi msaidizi wa kikosi cha zima moto Hamadi Dadi ameeleza walivyopata taarifa za ajali wametumia muda mrefu kufika katika eneo hilo la tukio,ingawa wametumia muda mrefu kuuzima huo moto kutokana na mafuta yaliyokuwa yakivuja.
Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo,na askari walionekana muda wote kwenye eneo la tukio.
No comments:
Post a Comment