Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Tuesday, February 17, 2015

CHELSEA YANUSA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA,HUKU BAYERN WAKISHIKWA NA SHAKHATAR

Usiku wa kuamkia Leo zilichezwa mechi mbili tofauti kwenye ligi ya mabingwa ulaya,maarufu kama UEFA. PSG alikuwa mwenyeji wa CHELSEA,na SHAKHTAR DONESTSK alikuwa mwenyeji wa BAYERN MUNICH.

Mechi kati ya PSG vs CHELSEA  ilimarizika kwa sare ya mabao ya moja kwa moja.Chelsea ilikuwa ya kwanza kuliona lango la wenyeji PSG kupitia beki mahiri kabisa Branislav Ivanovic mnamo wa dakika ya 36 ya mchezo.Kipindi cha pili PSG  walikuja kwa kasi na kuweza kusawazisha bao kupitia kwa mshambuliaji wao Edison Cavani kwenye dakika ya 54 ya mchezo.Kwa matokeo hayo inaipa nafasi kubwa Chelsea kusonga hatua ya robo fainali,kutokana na gori la ugenini

Kwenye mechi hiyo iliyopigwa kwenye uwanja wa PARC DE PRINCES uliohudhuriwa na magwiji kama Sir Alex Ferguson, David Beckham, na Michel Platin.

Kikosi cha PSG kilikuwa:-
Sirigu,van de wiel,Marquinho,Thiago Silva,Maxwell, Verratti,David luiz,Matuidi,Lavezzi/Pastored dk 81,Ibrahimovic na Cavan

Kikosi cha Chelsea kilikuwa:-
Courtois,Ivanovic,Cahill, Terry,Azpiculrueta,Ramirez,Matic,Willian/Cuadrado dk79,Fabregas/Oscar dk81,Hazard na Dieogo costa/Remy dk81.

Kwenye mechi nyingine kati ya SHAKHTAR DONETSK VS BAYERN MUNICH,zilitoka sare ya bira kufungana,huku Xabi Alonso akitolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu.Alonso alikuwa anacheza mechi yake ya 100 ya ligi ya mabingwa ulaya.

Timu hizi zitarudiana tarehe 11/3/2015,ambapo Chelsea itawakaribisha PSG  Stamford Bridge, na Bayern Munich itawakaribisha Shakhtar Donetsk

No comments:

Post a Comment