Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Shamariwa A,kata ya Igoma wilaya ya Nyamagana,jijini Mwanza,Julius Makoye (CCM), amekutwa amejinyonga juu ya mti ulio jirani na nyumba yake usiku wa Jana.
Makoye aliyetangazwa mshindi wa kiti hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba 14,mwaka jana,ameuongoza mtaa huu kwa awamu ya pili baada ya kuongoza miaka mitano iliyopita.
Mke wa marehemu,Ivona Polikalapo,alisema saa 10 jioni juzi alimsikia mumewe akiongea na mtu kwenye simu yake ya mkononi na kumsisitiza anahitaji mzigo wake wote.
"Jana (juzi) saa 10 jioni nilimsikia mume wangu akiongea na mtu na kutaka alipwe mzigo wake wote kutokana na kukaa mda mrefu,lakini aliyekuwa anaongea nae sikumfahamu ni nani."-Polilkalapo.
Aidha,alisema ilipofika saa 10 alfajiri ya jana,mbwa wao walisikika wakibweka kwa muda mrefu hali iliyomfanya marehemu atoke nje kuangalia kilichopo katika banda lao la mifugo la kuku(mke) akiendelea kuandaa chakula cha mifugo hao.
"Baada mume wangu kuamka na kwenda kuangalia kilichopo nje,hakuweza kurejea ndani hadi pale nilipotoka kumwaga uchafu shimoni nikashangaa baada ya kumuona ananing'inia juu ya mti,nipojaribu kumuita hakuitika ," alisema
Hata hivyo ,mama huyo anasema haamini kama mume wake amejinyonga bali kanyongwa kytokana na mti aliojitundika kutoonekana kuwapo na jiwe la sapoti,ili kutekeleza azma yake hiyo
No comments:
Post a Comment