Diva wa filamu nchini,Wastara Juma ambaye sasa anaripotiwa kuwa katika mapenzi na mwigixaji mwenzake, Bond Bin Suleiman anadaiwa kupoteza fahamu Mara tu baada ya kupewa taarifa kuwa mpenziwe huyo amepata mtoto wa nne kwa mwanamke mwingne.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Wastara aliyepenyezwa ubuyu na mpenzi wa zamani wa Bond,Lulu Semagongo"Aunt lulu" na kuambiwa kwamba asijishebedue kwani Bond ana mwanamke mwingne am aye amejufungua mtoto wa nne hivi karibuni.
"Tunakushangaa unavyojunadi kwa Bond ni wako na kumpa zawadi ya keki ya birthday wakati mwenzako amezaa na mwanamke mmoja baamedi hivi karibuni.Tena si kwamba mtoto huyo ni wa kwanza ,ni wa nne" kilisema chanzo hicho kikimnukuu Aunty.
Chanzo hicho kifunguka kuwa,baada ya kupewa taarifa hizo na Aunty Lulu,alizimia ghafra na kulazwa hospitali
" wastara alizimia punde tu baada ya kupewa taarifa hizo,nasikia walimkimbiza hospitali,akapewa huduma,ishu ilikuwa mbaya,Aunt Lulu alimchana live"
Risasi lilimtafuta Aunty Lulu ambaye awali alikuwa akilalamika penzi la kitumwa la kupigwa mara kwa mara na Bond na hata kufikiria mahali na kushukuru Mungu kwa kutengana kwao na kumuuliza kama habari hizo zilikuwa na ukweli wowote.
"Ni kweli nilimwambia kila kitu Wastara na tulipanga kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa ili kujua kama kweli ni wa bond.
"Mimi niliamua kufunguka baada ya Bond kunitukana na kunitolea maneno mazito kwani nilichoka kama amepata presha na kulazwa hilo mi sijui," alisema Aunt lulu.
Kwa upande wake,Wastara alikiri kupoteza fahamu na kulazwa hosptalini,lakini akakataa mambo hayo kumtokea kwa sababu ya jusikia taarifa hizo,bali kutokana name kuzidiwa na malaria.
"Nimepata nafuu na nimeshatoka hospitali nilikuwa ninepatwa na homa kali ya malaria, madaktari waliniambia nilikuwa na malaria 10 kwa muda wa wiki 2 nilikuwa naumwa,lakini nikszidiwa kidogo,hivi sasa niko uwanja wa ndege nashuka nikitokea Mwanza"alisema Wastara
No comments:
Post a Comment