Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Tuesday, February 17, 2015

KESI YA UGAIDI;,KIONGOZI WA JUMIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU AFIKISHWA MAHAKAMANI CHINI YA ULINZI MKALI

Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam,iliimarisha ulinzi wakati kesi ya ugaidi inayomkabili kiongozi wa jumuiya ya Uamsho na mihadhara ya kiislam Zanzibar(JUMIIKI).Shekhe Farid Hadi  Ahmed na wenzake ilipotajwa.

Askar walikuwa wengi katika eneo la mahakama huku kila mtu aliyeingia getini akikaguliwa kwa kifaa maalumu na kupapaswa ili kuangalia kama ana silaha.

Jana kesi hiyo ilitajwa mbele ya Hakim mkazi Janet Kaluyenda na kuahirishwa hadi march 4 mwaka Huu itakapotajwa tena.

Wakili wa serikali Peter Njike alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini bado wanasubiri uamuzi wa rufaa waliyokata katika mahakama ya Rufani.

Upande wa Jamhuri ulikataa rufaa kupinga uamuzi wa mahakama  kuu ya Dar es salaam ulioamuru mahakama ya Kiisutu kusikiliza na kutolea uamuzi hoja za washitakiwa

Washitakiwa wanadaiwa kati ya January mwaka juzi na juni mwaka Jana katika maeneo ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania,walikuwa na njama ya kutenda kosa kwa kutafuta watu wa kushiriki  vitendo vya ugaidi.

Katika mashitaka mengine wote wanadaiwa katika kipindi hicho,huku wakijua ni kosa waliokubaliana kuwainginza nchini  Sadick Absaloum na Faraha Omar washiriki vitendo vya ugaidi.

No comments:

Post a Comment