Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Thursday, February 19, 2015

WANASIASA WAHUSISHWA NA MAUAJI YA ALBINO NCHINI ..TANGU 2007 HADI SASA ALBINO 76 WAMEUAWA KIKATILI.

Wanasiasa wamenyooshewa vidole,wakihusishwa na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi baada ya matukio hayo kuhusishwa na harakati za kuelekea katika uchaguzi mkuu.

Vyama vya watu wenye ulemavu pamoja na baadhi ya wadau kutoka vyama vya siasa,vimetaka serikali kutopuuzia dhana hiyo ya kuhusisha harakati za kisiasa na mauaji hayo.

Aidha, Chama cha Walemavu wa ngozi Tanzania, kimesema kiko katika maandalizi ya kufanya maandamano ya amani hadi ikulu kwa ajili ya kumuona raisi Jakaya Kikwete wapange mikakati ya kutokomeza mauaji hayo ya ukatili.

Akizungumza katika mkutano uliandaliwa na shirikisho la vyama vya Walemavu  na vyama vya Siada nchini,mwamachama kutoka chama cha Wananchi (CUF),Abdallah alisema katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi,alisema albino wanaishi kwa wasiwasi kutokana na uwezekano wa mauaji hayokyanza kuibuka tena kwa kasi.

"Mimi mwenyewe Nina tatizo la ngozi (albino), hivi sasa tuko kwenye kipindi cha uchaguzi,na tetesi ni kwamba wengi wanauwa kwa imani potofu za baadhi ya wangu kutaka madaraka,tusaidieni jamani ukweli ni kwamba tunaishi kwa hofu.Alisema

Alisema ni vyema serikali ikaacha kupuuzia tetesi hizo za kuwahisisha baadhi ya watu wanaotaka madaraka na kuagiza watu wenye ulemavu wauawe kwa imani za kishirikina.

Alitaka hatua madhubuti zivhukuliwe kuokoa maisha ya Watanzania hao.

"Jamani tujue kuwa ni damu inamwagika  ni ya ndugu zetu,kama hatua zisipochukuliwa inaweza kuwa laana kwa vuzazi vyetu.Tukijipanga Tanzania tunaweza kuwa salama" alisisitiza.

Mwenyekiti wa chama cha wakulima  (AFP),Said Soud alisema jamii inatakiwa itambue  kuwa ni dhambi watu kufikiria wanaweza kupata utajiri  wa madaraka kupitia mauaji au viungo vya Albino.

"Hili naomba likemewe kwa nguvu zote,hii ni dhambi kubwa,sisi wanasiasa tututmie  majukwaaa kukemea dhambi hii,lakini pia serikali nayo itekeleze kwa vitendo sheria zilizopo na kuwaadhibu vikali  wale wrote wanaohusika na dhambi hii,"alisema.

USHIRIKINA.
Hivi karibuni katika semina iliyoandaliwa na Jumiya ya Serikali za Mitaa Tanzania(ALAT),baadhi ya washiriki walitaja uchaguzi mkuu kuchochea ongezeko la mauaji ya wenye ulemavu kutokana name wagombea kutumia mbinu chafu na dhaifu.

Katika semina iliyofadhiliwa na serikali ya Sweden kupitia shirika lake la Kimataifa la Maendeleo na Misaada (SIDA),ilielezwa na baadhi ya wachangiaji kwamba,ongezeko  la mauaji ya albino katika kipindi cha uchaguzi,linatokana na imani potofu  miongoni mwa wanasiasa uchwara.

Miongoni mwa wachangiaji katila semina hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam,Diwani wa Kata ya sunya,wilayani kiteto,Manyara,Mussa Brighton (CCM) aliyeomba serikali kutafuta mbinu za kudumu za kukabili wanasiasa wa aina hiyo.

Juzi,Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja huo (UNDP),ALVARO RODRIGUEZ katika taarifa yake kwa vyombo vya habari,pia aligusia kuwapo  taarifa zinazohusisha wanasiasa na mauaji hayo.

Maandamano.
"Kutokana na tatizo hili kuzidi kuwa sugu chama chetu kimeanza maandalizi ya maandamano ya amani na kupeleka kilio chetu kwa Raisi ili tuweze kushauriana utaratibu wa kupata suluhuya kudumu ya tatizo hili."alisema Kimaya.

Alisema katika maandamano hayo watafanya machi 2,mwaka huu na kwamba,pamoja na kupeleka kilio hicho kwa Raisi,pia watafanya sala maalumu kwa ajili ya wote waliopoteza maisha yao kwa kuuawa kikatili.

No comments:

Post a Comment