Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Tuesday, February 24, 2015

WAETHIOPIA 13 WAKAMATWA WAKISAFIRISHWA MOROGORO:

Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro limewakamata wahamiaji haramu 13 kutoka nchini  Ethiopia wakiwa kwebmnye gari dogo aina Prado katika kijiji cha Lusanga Turiani wilayani Mvomero wakijiandaa kwenda Afrika Kusini kupitia mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ACP Leonard Paul akizungumzua tukio hilo amesema waethiopia hao walitokea nchini Kenya na kupita Handeni na kuingia wilayani Mvomero na walikuwa wakijiandaa kwenda Mbeya kabla ya kwenda Afrika kusini.

Jeshi hilo linamshikilia dereva wa gari  hiyo na wanafanya mawasiliano na idara ya uhamiaji  na baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani .

Naye dereva wa gari ndogo aina ya Prado Musa Edmund akiongea huku akionesha kuficha sura yake anayeshikiliwa kwa kusafirisha waethiopia hao amesema akimpeleka boss wake Arusha njiani wakati anarudi alikutana na waethiopia hao,na wakakubaliana malipo yatafanyika pindi akiwa wafikisha mbeya

No comments:

Post a Comment