Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Tuesday, February 17, 2015

MAGAIDI WA TANGA WATIWA MBARONI MWILI WA MWAJESHI WA JWTZ ALIYEUWA KATIKA MAPIGANO HAYO WAAGWA.

Seriali imetoa taarifa rasmi kuhusu uhalifu  uliotikisa mkoani Tanga,ikisema hali ni shwari name umma wa watazania  upuuze taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikitia hofu.

Aidha inasema watu kadhaa wanashikiliwa wakihusishwa na uhalifu huo.

"Tunawashikilia ila mpaka sasa sowezi kukueleza idadi yao na kwamba ni wa kikundi cha ugaidi au la.Hao wangu tunafanya nao mahojiano ili kuweza kuelewa kama wanahusika kwenye tukio hilo.Alisema kamanda wa polisi mkoani Tanga Juma Ndaki

Alitoa taarifa kwa waandishi wa habari ,Ndaki alisema hali katika kitongoji cha majimoto,Amboni na mkoa wa Tanga kwa ujumla iko shear I;- "Tunaendelea kufanya uchunguzi kubaini hao wahalifu pamoja na silaha ziloibiwa" alisema

  "Tunaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano wao has a wanapoona wangu we ye majeraha au wanao wahisi kwamba ni wahalifu ili nasi tuweze kuwachunguza kama wanahusika kwenye tukio chili.Alisema

Ingawa kamanda hakueleza mazingira ya kukamatwa kwa watuhumiwa,waandishi wa habari waliozuru eneo la Amboni yalipptokea mapigano ,waliarifiwa kwamba baadhi ya wavuvi kwenye mto Zigi walimkamata mtu wakimtuhumu akifua nguo zenye damu.

Katika mapigano hayo baina ya askari na wahalifu yalisababisha kifo cha askari wa JWTZ ,sajenti Said Kajembe wengine kujeruhiwa.

"Asubuhi wavuvi kadhaa walikuwa hapo mtoni,ghafla walikutana na mtu pembeni ya mto akiwa anafua kanzu,pamoja na vifaa Fulani kama nguo za kufunikia uso,ikabidi wawapigie haraka polisi sumu lakini hawakuweza kupatikana na ndipo wakawapigia askari wa JWTZ ambao walifika fasta eneo tukio na kumkamata mhusika,Alisema mkazi mmoja wapo.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga,Magalula Saudi Magalula aliwataka wakazi wa Tanga na vitongoji vyake kuondoa hofu kwa kuhakikisha wanaendelea name shughuli zao za uzalishaji kwa sababu ulinzi umeimarishwa na halo ya usalama ni shwari.

Pia aliwataka wananchi na wageni wenye mpango wa kutembelea eneo la kihistoria a mapango ya Amboni,kuendelea na ratiba zao,kwasababu eneo hilo liko salama na tangu awali halikuhusika katika vurugu hizo.

Magula ambaye alikutana name wandishi was habari alisema:-
  "Hali ni nzuri,ulinzi na usalama UK imara,naomba wananchi waondoe hofu wawe na amani na waendekee name shughuli zao za uzalishaji.....hakuna tatizo kabisa usalama umethibitiwa vizuri"

Wakazi wazungumza.
Wakizungumza na waandishi,baadhi ya wakazi wa maeneo jirani na eneo hilo walisema hawajaruhusiwa kufika eneo hilo kwa kuwa inaendelea kulindwa na askari wa polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) na kushirikiana na JWTZ.

  "Muda mfupi tu kabla ya nyinyi kwenda huko askari wa FFU  walitoka huko,ninyi mnaelezwa kwamba pako shwari lakini sisi bado hatujaruhusiwa kufika kwa sababu panalindwa muda wote na askari"alisema mkazi alijejitambulisha kwa jina mmoja tu la Mrisho.

Katika hatua nyingne askari wa JWTZ aliyefariki waati akitibiwa katika hospitali ya Bimbo baada ya kujeruhiwa kwenye mapigano hayo mwishoni mwa wiki ,mwili wake uliagwa Jana mjini hapa kabla ya kupelekwa kwenye mazishi wilayani korogwe.

No comments:

Post a Comment