Wakati CCM kikijiandaa kuanza mchakato wa kupitisha jina la mgombea wake wa nafasi ya uraisi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu,imeelezwa kwamba hali si shwari ndani ya chama hicho kutokana na kile kinachodaiwa,mkakati wa baadhi ya viongozi kubeba name kukumbatia watu wao kwa lengo la kulinda masilahi binafsi.
Chanzo chetu cha kuaminik kutoka ndani ya CCM kimeeleza kuwa joto kubwa linazidi kufukuta kuelekea mchakato wa kupata jina la mgombea kutokana na Tabia za baadhi ya viongizi kupigia debe majina na watu wanaomini wakishinda watanufaika nao kwa kulinda masilahi binafsi.
Akizungumza na WAKEREKETWA jana,kwa sharti la kutoandikwa jina,mmoja wa makada maarufu wa chama hicho ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM ( NEC-CCM),alisema kuna mgawanyiko mkubwa miongoni mwa vigogo wa cham hicho kupata jina la mginbea wa uraisi hali anbayo inasema ina kila dalili za kusambaratisha chama hicho.
"Kuna tatizo katika kupata jina,tena ni tatizi kubwa,tatizo hili lipo kwa baadhi ya viongozi wa chama chetu kila mmoja anatembea na jina la mtu wake mfukoni.Wanahangaika kujipitisha huku na Kule kwa visingizoo mbalimbali huku mkono mwingne wakupitidha ajenda za kunadi watu wao.
Hatutakubaliana na chili!,wana CCM waachwe wamue! Sio kuleteana makina kwa ujanja hapa" alilalamika kada uyo na kuongeza.
"Hata Pinda ( waziri Mizengo Pinda )juzi akiwa Iringa,ameonya tabia ya viongozi kutaka kuwachaguliwa wananchi viongozi.Pinda hakutoa kauli hiyo hewani bali anajua kinachofanyika."
'Wanafikiri hatujui kila mmoja ana mtu wake wanahangaika uaiku na mchana,sisi tunawasubiri wakifanta kosa katika hili wataona matokeo take,CCM itameguka vipande vipande,"
Alishauri vikao vote vya maamuzi ndani ya chama kutenda haki na kupitisha mtu kwa sifa na rekodi na maadili yake katika kuwatumikia wananchi.
Alisisitiza kuwa shuguli ya kupitisha jina la mgombea wa CCM inapaswa kufnywa na tahadhari kubwa na kuomba viongozi wakongwe wa chama hicho wakiwemo mzee Ali Hassan Mwinyi,Benjamin Mkapa,John Malecela,Pius Msekwa na Amani karume kusaidia kubaini kushawishi na baadae kupitisha majina wangu wanaofaa kubeba jukumu hilo.
"Mimi nashauri tena kwa msisitizo,viongozi watakaosimamia mchakato Hui watende haki,wafuate kanuni,wazingatie sifa 13 za mgombea was uraisi. Kwa hili kuna mtu sitaki kumnyima khaki yake,lazima nimsifu ,huyu ni Comredy Mangula (Phillip-makamu mwenyekiti wa CCM TANZANIA bar a)
Kada Hugo alishauri wana CCM wenye sifa kujitokeza bila uwoga kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo uraisi muda utakapofika
No comments:
Post a Comment