Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Friday, February 20, 2015

LOWASSA AZIDI KUSHAWISHIWA ATANGAZE NIA YW KUWANIA URAISI

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kishapu  Mkoani Shinyanga,Shija Ntelezu,amwungana name baadhi ya wana CCM wengine kumuomba waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa,ajitojeze kutangaza nia ya kugombea uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake juzi,Ntelezu alisema kwa niaba ya wana kishapu wenzake watano ni wakati mwafaka hivi sasa wa kutangaza nia yake kugombea nafasi hiyo ili ampokee kijiti Raisi Jakaya Kikwete.

Mwenyekiti Huyo amasema kwa kadri anavyomfahamu Lowassa ni mmoja wa viongozi wachapa kazi wazuri hapa nchini na mwenye uwezo kutoa maamuzi magumu yanapohitajika kutolewa na kwamba ndiye kwa sasa anayeweza kumrithi Raisi Kikwete na kuendeleza kasi ya kusukuma kasi ya maendeleo aliyoyaanza.

Alisema wakati taiga likielekea kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu,oktoba mwaka huu ni muhimu CCM kikawa Makini kuhakikisha kinamteua mgombea mwenye uwezo was kukabiliana na wagombea waupinzani.

"Sisi Kishapu tunaamini iwapo CCM itamsimamisha mgombea jasiri mwenye uzoefu wa kiongizi ambaye pia ana historia nzuri ya uchapa kazi hapa nchini ambaye haitokuwa kazi kubwa kumnadi kwa wapiga kura nafikiri Lowassa anatosha kwa nafasi hiyo hivi sasa,yapo mambo mengi makubwa aliyafanya wakati wa uongozi wake,"

"Utumishi wa Lowassa unafahamika hapa nchini kuanzia ndani ya chama hadi serikalini,kwa sisi wa Shinyanga tunamfahamu zaidi maana aliwahi kuwa mtendaji wetu enzi ya TANU,lakini kikubwa tunachokikumbuka ni jinsi alivyoweza kutufanikishia mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoria" alieleza Ntelezu.

Alisema ni muhimu vikao mbalimbali vya uteuzi ndani ya CCM  vikawa makini katika kufikia maamuzi yake na wajumbe wake wasikubali kuyumbishwa na maneno ya watu wasiokitakia mema chama hicho  na kwamba kimchunguze kwa umakini kila mgombea aliyojitokeza bila ya jump aka sifa mbaya za uongo.

Mwenyekiti  huyo alifafanua kuwa ushauri wao wa kumtaka Lowassa agombee nafasi hiyo ya uraisi si kwamba wana CCM wengine waliojitokeza hawana sifa hizo,bali ni muhimu kumpa kipaumbele mtu mwenye uzoefu mkubwa kwa kiutendaji ndani ya serikali na chama.

"Ushauri wetu usichukuliwe kwamba wana CCM wengine waliokwisha tangaza nia hawafai au hawana uwezo na hakuna anayewalaumu,maana ni haki yao ya kikatiba,lakini tunaangalia ni yupi miongoni mwao mwenye uwezo zaidi atakayeweza kukivusha chama chetu kwa urahisi kwenye uchaguzi mkuu ujao" alieleza.

Lowassa pamoja na makada wengine watano,Fedrick Sumaye,William Ngeleja,January Makamba,Bernard Membe na Stephen Wassira  juzi walimaliza kifungo cha miezi 12 walichopewa na kamati kuu ya CCM ikawa ni adhabu ya kukiuka kanuni na taratibu za chama hicho na kuanza kampeni za kuwanua uraisi kabla ya wakati.

No comments:

Post a Comment