Ajali mbaya imetokea Changalawe Mafinga basi la majinja limeaangukiwa na kontena mida ya mchana,inasemekana karibia wote wamefariki waliokuwemo kwenye basi hilo. Mungu azilaze roho za marehe mahali pema peponi. Amina
Updates:-
Taarifa za awali kutoka kwa jeshi la Polisi mkoani Iringa zinasema basi la kampuni ya Majinja lilolaliwa na Lori lilokuwa limebeba jumla ya watu 49, idadi hiyo ni pamoja na dereva na kondata,wengi wao wamepoteza maisha na idadi ya majeruhi kama wamepatikana bado haijajulikana.
Pia Jeshi la Polisi limesema wamekuta madaftari mengi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaaam. Hivyo basi wanaendelea kufanya uchunguzi na kumuhoji mmiliki wa basi hilo kama basi hilo lillikodishwa na wanafunzi hao wa chuo Kikuyu cha Dar es Salaaam.
No comments:
Post a Comment