Staa wa bongo muvi na fleva ,Shilole amedaiwa kutaka kumpiga tens mpenzi wake ambaye pia ni msanii Nuh Mziwanda kwa chupa hivi karibuni wakiwa kwenye sherehe ya meneja wake Kajala ,aitwaye Lamata iliyofanyika pande za Samaki samaki Posta Jijini DAR.
Katika tukio hilo,habari zinasema kuwa Shilole alikuwa amelewa sana na kwamba walikuwa wamekaa sehemu tofauti na Nuh Mziwanda ghafla sehemu aliyokuwa amekaa Nuh na wasanii wengine ili rushwa chupa ambayo ilikuwa ikimlenga msanii huyo,kwa bahati nzuri aliikwepa na kumpiga jamaa mwingine lakini haikumuumiza.
Baada ya tukio hill ilibidi baadhi ya wasanii wengine wamjie juu Shilole na kumuuliza kwanini alitaka kumpasua Nuh,Shilole alianzisha ugomvi na kuzua tafrani kwebye sherehe hiyo na baadaye akaamua kukaa pembeni peke yake na kuanza kulia.
"Yaani unaambiwa kama ile chupa ingempata Nuh sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine,alikuwa anamjeruhi vibaya sana kiukweli alileta fujo kwenye sherehe ile" alisema mmoja ya watu waliokuwa kwenye sherehe hiyo.
Baada ya hapo msanii Quick Racker alimfata Shilole na kumwambia kuwa kumbe akilia anakuwa mbaya ndipo aliamka na kumrushia chupa Quick Racker kwa bahati nzuri aliikwepa.
Hata hivyo Soudy Brown alipompigia simu Shilole kumsomea mashitaka hayo alimwambia asimsumbue kwani muda huo alikuwa amelala.
Shilole amekuwa akimpiga na kumdhalilisha mpenzi wake Nuh hadharani mara kwa mara katika vipindi vya karibuni. Ikumbukwe Shilole alimzaba vibao Nuh Mziwanda kwenye tamasha la muziki la Tigo lilofanyika pale leaders na baada ya tukio hilo Shilole alimuomba radhi mpenzi wake kwenye vyombo vya habari na kuhaidi kutompiga tena.
No comments:
Post a Comment