Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Thursday, February 19, 2015

KORTINI KWA TUHUMA ZA KUNUNUA "MALAYA" WA BUGURUNI ROZANA.

Wangu wanne wamefikishwa katika mahakama ya Jiji kwa tuhuma za kununua machangudoa katika eneo la Buguruni Rozana jijini Dar es salaam.watuhumiwa  hao waliofikishwa  Jumanne ya wiki hii katika mahakama hiyo ni Antidius Severian (25),Yaham Mihamed (24),Ally Hassan (35) na Mohammed Hamis (27).

Wakisomewa mashtaka na wakili wa serikali,Ramadhan Kalinga mbele ya Hakimu Mkazi  Mfawidhi Bernard Mpepo,alidai kuwa  February 14,mwaka huu katika  eneo la Buguruni Rozana watuhumiwa hao walikamatwa na askari mwenye namba E.7882D/CPL wakifanya manunuzi ya madada poa  huku  wakijua ni kosa kisheria.

Hata hivyo,washtakiwa hao walikana kosa hilo,ambapo Hakimu Mpepo,alisema dhamana kwa watuhumiwa hao ipo wazi ambapo aliwataka kila mmoja na wadhamini wawili ambao kila mmoka atasaini dhamana ya Tsh 200000.

Watuhumiwa hao walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi February 24 ,mwaka huu kesi itakapotajwa tRNA.

No comments:

Post a Comment