Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Thursday, February 26, 2015

BREAKING NEWS: CHIDI BENZI AHUKUMIEA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI JELA:

Mwanamziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashid Abdalah Makwaro maarufu kama (Chidi Benzi) amehukumiwa  kifungo cha miaka miwili  jela au kulipa faini ya shilingi 900000 kwa kosa la kutumia madawa ya kulevya na bangi.

Chidi Benzi alikamatwa uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam,akiwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya 38000,bangi zenye thamani ya 1700, pamoja na vifaa vya kutumia madawa ayo.

Chidi Benzi alikiri kosa mbele ya mahakama kuwa ni mtumiaji wa madawa hayo. Baada ya mahakama kusikiliza pande zote mbili ikamkuta Chidi Benzi ana hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Tsh900,000/=

Wimbi la wasanii wanaotumia madawa ya kulevya linazidi ongezeka,nguvu kazi za taifa zinazidi kupotea lakini hii yote inasababishwa na waingizaji na wasabazaji wa haya madawa nchini

No comments:

Post a Comment