Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Monday, February 16, 2015

ASKARI SITA WAMEJERUHIWA VIBAYA KATIKA MAPIGANO YA UKO TANGA BAINA YA KIKUNDI CHA MAGAIDI

Askari sita wakiwemo wanne wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ),wamejeruhiwa vibaya  kwa risasi wakati was mapigano,baina yao na watu wanaodhaniwa kuwa ni  wahalifu wakati wa msako msalimie wa kutafuta silaha zinazodaiwa kufichwa kwenye mmoja ya eneo la mapango ya Amboni.
Kamishina wa Operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi PAUL CHANGONJA,amebainisha hayo Alasiri  ya jana,wakati akitoa taarifa kwa wanahabari jijini Tanga kuhusu hali ya matukio ya uhalifu yanayoendelea jijini humo.
Alisema mapambano hayo yaliyotokea muda mfupi tu,wakati wa msako maalumu wa kutafuta silaha zinazodaiwa kufichwa kwenye mmoja ya eneo la mapango ya Amboni,yaliyopo umbali wa kilomita 10 kutoka kijiji la Tanga.
"Baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa wasiri wetu ndipo alfajiri ya leo(jana).Askari wetu walienda eneo kitukio kwa lengo la kutafuta hizo silaha na gafla wakavamiwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana waliokuwa wamejificha"Alisema
Alisema kujeruhiwa kwao kumetokana na mapambano ya kurushiana risasi yaliyodumu kwa dakika 15  alfajiri ya kuamkia jana katika mashimo ya mawe ambayo yapo jirani na mapango ya Amboni.
Kamishina Changonja alisema chanzo cha mapambano hayo ni tukio la Januari 26 mwaka huu wakati Askari wawili walipovamiwa na wangu wasiojulikana na kunyanga'anywa bunduki mbili aina ya SMG,zilizokuwa na risasi 60.
"Upelelezi wetu uliendelea baada baada ya tukio kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kuwasaka na tukafanikiwa kupata wahalifu.Jana asubuhi tuliarifiwa kwamba silaha hizo zimefichwa kwenye mmoja ya mapango ya Amboni name ndiko wakapeleka Askari uko ili kuzitafuta"alisema
"Wakati askari wakiendeleaa kuzitafuta,gafla walivamiwa kwa kupigwa risaso na waliokuwa  wamejificha kwenye eneo lingine LA pango hilo,ikalazimika wajibu mapigo"Alisema
Kamishina Kagonja alisema baada ya kuzima mapigano,waliamua kuingia ndani ya mapango hayo na  kukuta vifaa mbalimbali vya kutengenezea milipuko,pikipiki moja,baiskeli tatu,silaha mbalimali za jadi zikiwemo  mishale pinde ,visu na mapanga lakini hawakufanikiwa kukuta mtu.
Akizingumza kuhusu watu hao kwamba ni kikundi cha wahalifu wa Alshabaab au la,alisema mpaka sasa polisi hajabaini kutokana na ukweli kwamba katika operesheni hiyo hawajafanikiwa kukamata mtu amabaye wanaweza kumfananisha na magaidi hao.
"Msako with unaendelea tunaomba wananchi watoe ushirikiano kwa ukweli ni mapema sana kuthibitsha kwamba hao wahalifu ni wa kikundi cha Al-shabaab kama inavyodaiwa mitaani,kwasababu mpaka sasa hatujatambua sura Zao na kubaini ni watu wa aina gani"Alisema
Alisema askari waliojeruhiwa,wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga ya Bombo na hali ya afya zao zinaendelea vizuri

No comments:

Post a Comment