Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Wednesday, February 25, 2015

"POLE CHRIS BROWN MWENZAKO NILICHEKWA "- OMMY DIMPOZ

Msanii Omary Nyembo alimaarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kusema kuwa watu wa uhamiaji duniani kote huwa hawatambui umaarufu wa MTU pindi wanapogundua kuna kitu hakijienda sawa, Ommy Dimpoz amefunguka hayo leo kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya mwimbaji kutoka Marekani  Chris Brown kuzuiliwa kuingia Canada na kusababisha kusitishwa kwa show zake mbili alitakiwa kuzifanya Canada ndani ya wiki hii.

Ommy Dimpoz ameonyesha jinsi gani watanzania na mashabiki wake walilipokelea suala lake tofauti na kuonyesha kuwa watu wengi walimcheka na kumchamba kuwa yeye ni mtu maarufu  hivyo asingeweza kupatwa na suala hilo.

"Pole braza Kristofa, haya ni mambo ya kawaida Ila mwenzio nilivyozuiwa kuingia nchini kwenu basi nilivyorudi kwetu nimechekwa ,nimechambwa khaa,hawajuagi mambo ya Uhamiaji hawajali we nani"

Wiki ya wapenda nao msanii Ommy Dimpoz alirudishwa Tanzania baada ya kuzuiwa kuingia Marekani kwa kosa vibali vinavyomruhusu kuingia nchi hiyo kufanya  show.

No comments:

Post a Comment