Msanii anayefanya vizuri kunako bongo movie, Jacob Steven maarufu kama JB, hivi karibuni amejwaa scandal mpya ambayo inamshushia heshima kama sio kumpunguzia credit ndani ya tasnia hiyo.
Msanii huyo maarufu amekumbwa na skendo hiyo baada ya muvi yake mpya kutoka inayifahamika kwa jina la MZEE WA SWAGA.
Muvi hiyo inayofanya vizuri sokoni inasadikiwa kukopiwa na kupesti kama ilivyo na moja ya muvi maarufu kutoka Bollywood inayofahamima kwa jina la "LADIES VS RICKY BAHL".
Akizungumza kupita kipindi cha take one,Zamaradi Mketena amethibitisha usanii huo uliofanyika na kampuni maarufu ya JERUSALEM inayomilikiwa na JB,kuwa karibia scene zote zilizochezwa na Filamu ya Mzee wa swaga, imeiga kama ilivyo kuanzia stori hadi idadi ya waigizaji wakuu kutoka kwenye filamu hiyo ya kihindi iliyotoka mwaka 2011.
Mtangazaji huyo amelaani vikali utapeli huo uliofanyika na kampuni ya JB huku akijifanya yeye ndo mtunzi na mwandishi wa stori hiyo wakati ukweli anaujua mwenyewe.
No comments:
Post a Comment