Mamlaka ya mawasilano nchini,TCRA imetoa tamko kuhusiana na malalamiko kutoka kwa watumiaji wa huduma za sumu chini kufuatia kubadilika kwa vifurushi vya mawasiliano.
Malalamiko hay yalikuja baada ya baadhi ya mitandao ya simu kupunguza ukubwa wa data anazopata mtumiaji wa simu anapojiunga na vifurushi vya muda wa maongezi,sms na data kwa pamoja.
Baadhi ya mitandao imekuwa ikitoa Mega Bytes 8 peke yake ambazo kwa matumizi ya kawaida ni ndogo mno.
Mkurugenzi mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Pofesa John Nkoma kwenye taarifa yake na vyombo vya habari iliyotolewa leo jumanne,alisema.
"TCRA imechambua mpangilio wa vifurushi tozo za zamani na mpya na kugundua kwamba ingawaje baadhi ya watoa huduma wamebadlisha bei,kwa ujumla bei za muda wa kuzungumza na idadi ya meseji hazikubadilika sana.Hata hivyo,kuna upungufu mkubwa kwa idadi ya unit za data"
Kupitia kifungu cha 5 cha kanuni za tozo (EPOCA TARRIF REGULATIONS) za mwaka 2011,TCRA imeyataka makampuni ya simu kuwasilisha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania gharama mpya wanazokusudia kutoza wateja wao kabka haxijaanza kutumika. Pia imeyataka kupitia upya bei na tozo mpya kwa kuzingatia mapendekezo hayo na kuwasilisha kwa Mamlaka kama inavyotakiwa kwa mujibu wa kanuni za EPOCA za 2011 kuhusu tozo.
"TCRA inawaagiza watoa huduma kuhakikisha kwamba mabadiliko yoyote yanatejekezwa kidogokidogi na sio ghafla ili kuepuka sintofahamu katika soko," imesema.
"TCRA inaawaagiza watoa huduma kuwapa nafasi wateja wao ya kuchagua mpangilio wa vifurushi tofauti jwa huduma wanazohitaji.Meseji na Interneti cha siku,siku 7 au mwezi ambacho kinampa mtumiaji Uhuru was kuchagua kiasi ambacho wako tayarib kulipia kwa mazungumzo,meseji na intaneti"
Katika hatua nyingine taarifa hiyo imetoa takwimu ya kuongezeka kwa matumizi ya simu na intaneti nchini kwa kipindi cha miaka 10.imesema hadi sasa kuna laini za simu za mkononi zipatazo 31,862,656 ukikinganisha na laini 2,963,737 mwaka 2005.
"Idadi ya simu za mezani ni 151,ukilinganisha na 154,420 mwaka 2005. Watumiaji wa intaneti wameongezeka hadi jufikia 11,000,000 Desemba 2014 kutoka 3,563,732 mwaka 2008. Kwa sasa,kuna hamu kubwa ya matumizi ya intaneti na mwelekeo huu utaendelea; hasa kutapokywa na ongezeko la mitandao inayowezesha kutoa hyduma za intaneti,na kuongezeka kwa mitandao ya kijamii." Imesema.
"Wateja walionunua laini au ambao wanatumia huduma za sumu kwa kuzungumza imeongezeka kwa 91% kutoka million 3 mwaka 2005 hadi milion 32 mwaka 2014.Hii imewezesha huduma za simu kufikia 97% ya watanzania ilipofika Desemba 2014 kutoka 10% mwaka 2005 .
No comments:
Post a Comment