Takribani miaka 15 imepita tangu ilipotokea ajali katika kijiji cha Idweli wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya,iliyosababisha vifo vya watu walioungua wakichota petroli kwenye gari lililopinduka.
Hata hivyo,tukio la namna hiyo limejirudia tena kijijini hapo na safari hii watu wawili,wamekufa na wengine 18 kujeruhiwa wakati wakichota mafuta kwenye gari lililopinduka.
Lori hilo lilikuwa likisafirisha mafuta kutoka Dar es salaam kwenda Malawi.Lilipinduka kijijini hapo juzi.
Vifo hivyo viwili vya wakazi wa kijiji hicho,Maria Pajela(18) na William Paschal (38),vimetonesha makovu ya huzuni ya ndugu na jamaa wapatao 40 waliopoteza maisha na kulazimu miili yao kuzikwa kaburi moja,kutokana na kuharibika zaidi na kushindwa kitambuliwa.
Akitoa taarifa juu ya ajali ya juzi saa 3 usiku,Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema waliofariki na waliojeruhiwa,walikuwa katika harakati za kuiba mafuta kutoka katika gari aina ya Scania yenye namba za usajili T 891 AQZ likiwa na tela lennye namba T 821 ARF.
Alisema gari hilo Mali ya Ailis Sanga,lilipakia petroli yenye ujazo wa lita 41,000,kutoka Dar es salaam kwenda Malawi.
Lilikuwa likiendeshwa na Zawadi Nyato (46) mkazi wa Sae jijini Mbeya akiwa na utingo wake, Frank Yohana (24) mkazi wa mbozi.
Baada ya kufika kijijini hapo,liliacha njia na kupinduka.Dereva na utingo waliokolewa na kupelekwa kituo cha polisi kiwira kupata fomu namba tatu kwa ajili ya matibabu.
Kamanda alisema baadhi ya wakazi,walivamia Lori hilo na kutoboa tangi la mafuta,hali iliyosababisha mafuta kuanza kumwagika na kusambaa maeneo mbalimbali ikiaemo kwenye makazi ya watu.
No comments:
Post a Comment