Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Tuesday, February 17, 2015

RAISI KIKWETE AONGOZA MAZIKO YA CHIFU MKWAWA AMBAPO MWANAFUNZI WA MIAKA 13 ALIYETAWAZWA KUWA CHIFU MPYA WA WAHEHE

Mwanafunzi was darasa la saba,Adam Abdul Sapi Mkwawa ,ametawazwa kuwa chifu mpya ya wahehe,akirithi nafasi ya baba yake,aliyefariki na kuzikwa  mkoani iringa.

Raisi Jakaya Kikwete alishiriki maziko ya chifu huyo wa wahehe  Abdul Sapi Mkwawa(66) yaliyokwenda sanjuri na haafla ya kumsimika mtoto huyo kushika wadhifa huo  wa kimila.

Maziko ya kiongozi huyo aliyefariki  February 14 mwaka huu yalifanyika kijiji cha Kalenga nje kidogo name mji wa iringa  ndani ya makumbusho yaliyowekwa fuvu la babu yake chifu Mkwavinyika Munyigumba  Mwamunyinga Mkwawa

Mbali na Raisi  Kikwete wengine waliohudhuriwa maziko hayo ambayo taratibu zake zilitumia takribani SAA 2.30 kuanzia SAA 7 saa 7 mchana ni pamoja na mkuu mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM)  kwa upande wa Tanzania Bara Phillip Man gala,wakuu wa mikoa ya Tanga na Mbeya na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya  siasa.

Kabla ya kifo choke kilichosababiswa na maradhi ya figo,Abdul Sapi Mkwawa aliyekuwa mtoto watatu wa spika wa kwanza mweusi nchini Adam Sapi

Kabla ya maziko ya chifu huyo,wazee wakabila la wahehe walimsimika Adam ambaye ni mtoto wake watano kuwa chifu mpya kabila hilo.

Hata hivyo,mtoto huyo anayesoma katika shule ya msingi ya Highlands ya mjini Iringa ,atalazjmika kusubiri kufanya shughuli za kichifu mpka atakapo timizwa umri wa miaka 20.

No comments:

Post a Comment