Msanii wa Bongo Fleva,Omary Nyembo "Ommy Dimpoz"amesema anashangazwa na uvumi unaoendeleaa kuwa yupo katika uhusiano na mwgizaji wa filamu,Wema Sepetu.
Akieleza kuhusu picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii,Ommy Dimpoz,alisema walikuwa Afrika Kusini ndipo picha hizo zilipopigwa.
" Tunapiga picha nyingi sana name Wema hats ukigoogle utaziona,hii siyo mara ya kwanza,lakini sijui kwanini hizi zimetengeneza taswira nyingine kwa mashabiki,".alisema
Ommy alisisitiza kuwa yeye hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenz na Ex wa rafiki yake,na kuwa yeye na Wema walikuwa wakifahamiana hata kabla ya Wema kuanza mahusiano na diamond.Hivyo kuachana kwao haiwezi kumpelekea yeye awe mbali nao kwani hayo ni mambo yao binafsi.
Japokuwa Ommy anaaamini kuwa kwenye pitapita za kimaisha inawezekana mtu akawa na mahusiano ya kimapenzi na Ex wa rafiki take,kwani hicho kitu kinawezekana
"Ku-date na Ex wa rafiki yangu,kwa mimi hapana,lakini kuhusu maswala ya kimapenzi lolote linaweza kutokea kwasababu umeshasema Ex kwa hiyo it means hawapo kwenye mahusiano tena,na pia inaweza kutokea huko mbele mbele maisha yameendelea watu wakaja kukutana,kwa hiyo vitu hi yo vinawezekana". Alisema.
Picha za wawili hao wakiwa ktika pozi tofauti zimeendelea kuwa gumzo na kuzua maswali mengi kwa mashabiki ,kutokana na ukaribu alionao Tommy na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Wema ,Diamond.
No comments:
Post a Comment