Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Tuesday, February 24, 2015

WANAJESHI 6 WA JKT WALIOTAKA KUANDAMANA WAFIKISHWA MAHAKAMANI CHINI YA ULINZI

Wahitumu sita wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taiga (JKT), wamepandushwa kizumbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kufanya mkusanyiko usio halali.

Washitakiwa hao ni Mwenyekiti wa Umoja wa wahitimu hao George Mgoba,Makamu Mwenyekiti Pataki Kiwango,Katubu Linus Steven,na wahitumu wengine Emmanuel Mwasyembe,Ridhuwani Ngowi na Jacob Mang'itwa.

Wote walikana mashitaka na kurudishwa rumande kwa kuwa Mkuegenzi wa Mashitaka (DPP) amewasilisha hati ya kuzuia dhamana dhidi yao.

Wakifikshwa mahskamani hapo asubuhi na jupandushwa juzumbani saa 10 kasoro jioni,wakikabiliwa na mashitaka matatu ya kula njama,kufanya mjusanyiko ysio halali na kushawishi wenzao kutenda kosa la jinai.

Wakili wa serikali,Nasoro katunga akisaidiwa na Tumaini Kweka,Hellenic Moshi,Janethroza Kitali na inspekta Jackson Chidunda ,alidai mbele ya Hakimu Mkazi,Frank Moshi kuwa Februari 15 mwaka huu katika eneo la Msimbazi centre,Ilala Dar es Salaam washitakiwa walipanga njama za kutenda kosa.

Alidai siku hiyo katika eneo hilo,walifanya mkusanyiki usio halali kwa lengo la kuandamana kwenda kwa Raisi kulazimisha wapewe ajira katika utumushi wa umma,jambo ambalo ni kinyume cha sheria na lingesababisha uvunjifu wa amani.

Katika mashitaka yanayowakabili akina Mgomba na wenzake,wanadaiwa siku hiyo katika eneo hilo,walishawishi wahitimu wenzao wa mafunzo ya JKT ,kufanya maandamano kwenda kwa Rais kulazimisha wapewe ajira katika utumishi wa umma jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Walikana mashitaka yanayowakabili na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi haujakamilika.DPP anewasilisha hati ya kuzuia dhamana dhidi yao,chini ya kifungu cha 148(4) cha mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).

No comments:

Post a Comment