Wakazi wa Ilula Mkoani Iringa wamegoma kupokea maiti ya mama aliyekuwa wakati wa mapambano yaliyotokea juzi mkoani humo kati yao na Polisi kwa masharti mawili.
MOSI : Wananchi 18 waliokamatwa na Jeshi la Polisi baada ya vurugu hizo waachiwe huru Mara moja bila masharti yoyote.
PILI: Polisi walio sababisha mauaji hao wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria.
Katika tukio hilo wananchi wa ilula walimtuhunu polis I kumuua mwanamke kwa kosa la kuuza pombe muda wa kazi na hivyo kupanda gadhabu na kuvamia kituo cha polisi ambako walichoma magari matano madogo na basi moja na baadae kwenda kufunga Barabara ya Dar es Salaam - Mbeya kwa muda wa masaa 5.
No comments:
Post a Comment