Wafanyabiashara watatu,na watano wanepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singinda wakikabiliwa na mashitaka ya kumdharirisha kupindukia askari polisi wa kike na kumsababisha maumivu makali mwilini
Mwanasheria wa serikali Petrida Mutta alidai mbele ya Hakimu Joyce Minde kwamba kwa pamoja eashitakiwa hao walimfanyia unyama askari huyo na kumvua nguo zote na kumwacha mtupu kisha kumshambulia na kusababisha maumivu makali mwilini.
Washitakiwa ni Jasmini Idd (40), Abdalah Handini (26), Ramadhani Bakari (32) wote ni wafanya biashara mjini hapa pamoja na dereva Said Said (50) wengine ni Aurelia Adolf Mushi (20), Grace David Paul (21), Happiness Kiluvya (23), Jackline John (20), Consolata Masaki (21) wote wanadaiwa ni wanafunzi wa elimu ya juu (chuo) cha mkoani hapa Singida.
Mwanasheria wa Serikali alidai wakati wote kitendo hicho cha udhalilishaji Polisi huyo alikuwa akichukuliwa picha za video huku akiwa mtupu na kuzisambaza mitandao ya kijamii.
Tukio hilo linadaiwa lilifanyika Februari 14 mwaka huu,saa 11:30 jioni amabako kwa mujibu wa mwendesha mashtaka inadaiwa Polisi huyo wa kike alikutwa akiwa name mume wa mshitakiwa Jasmin wakiwa kando ya ziwa Singidani wakijivinjari siku ya wapenda nao.
Mutta alidai mbele ya Mahakama Kuwa kitendo walichofanya washitakiwa ni kinyume cha kanuni ya Adhabu 138A kifungu cha 16, cha mwenendo wa makosa ya jinai.
No comments:
Post a Comment