Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Thursday, February 19, 2015

UGAIDI TANGA:WASOMALI WAWILI WATIWA MBARONI

Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na Jeshi la wananchi Tanzania ( JWTZ ),limewatia mbaroni watuhumiwa wawili wanaodaiwa kuwa name asili ya Somalia katika msako unaondelea dhidi ya kundi la wahalifu wa silaha mkoani Tanga.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi mjini hapa,kimeiambia MKEREKETWA kuwa watu hao walikamatwa jana saa 5 asububi katika eneo la kijiji cha Amboni Mafuriko,baada ya kuonekana katika eneo hilo wakiwa wanashangaa na hawajui wanapokwenda.

Baada ya kuonekana kwa watu hao,wananchi wa kijiji hicho kilicho jirani na kijiji cha Mleni ambako kundi la wahalifu wa silaha lilijificha,walitoa taarifa kwa polisi ambao walifika na kuwatia mbaroni.

"Ni kweli leo ( Jana ) saa 5 asubuhi huku eneo la kijiji cha Amboni Mafuriko kuna watu wawili wenye asili ya Somalia walikamatwa baada ya wanachi kuwaona na kuwatilia shaka,na hivyo kufanikisha kukamatwa", kilisema chanzo hicho.

Wakati huo huo,Jeshi hilo liliwashikilia watu wawili ambao ni wafanya biashara na waumini wa dini ya kiislamu wa jumuiya ya ANSWAR SUNI mkoani hapa,kwa tuhuma za kuhusishwa na tukio la kufadhili vikundi vya uporaji wa silaha dhidi ya Polisi.

Wakizungumza na mwaandishi wa habari hizi,ndugu wa watuhumiwa hao walidai ndugu zao walikamatwa na Polisi siku 3 zilizopita.

"Kuna ndugu zetu wawili wameshikiliwa kwa mahojiano kwa zaidi ya siku 3 na hatujawahi kuwaona kila tukiwapelekea chakula na dhamana imekataliwa hivyo hali hiyo inatupa wasiwasi mkubwa," alisema mmoja wa ndugu watuhumiwa hao ambae akutaka jina lake litajwe.

Mbali na matukio ya kukamatwa watu hao, hali ya ulinzi katika hospitali ya BOMBO imeimarishwa,hasa katika wodi ambao askari waliojeruhiwa kwenye tukio la Amboni wakiendelea na matibabu.

Wakereketwa ilipomtafuta kamanda wa Polisi,Fraser Kashai pamoja na kamishina Chagonja,wote walisema wapo katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama.

No comments:

Post a Comment