Mashabiki wa Arsenal jana ilikuwa siku chungu kwao baada ya kuishuhudia timu yao ikipigwa kipigo kitakatifu na timu ya Monaco inayoshiriki ligi kuu Ufaransa.
Mpaka mpira unamalizika matokeo yalikuwa ni Arsenal 1 vs 3 Monaco. Safu ya ulinzi wa Arsenal ilikuwa mbovu zaidi iliyomfanya nyota wa zamani wa Manchester United kuonekana mwiba wa kuotea mbali kwa kuisumbua sana ngome ya Arsenal
Wenger aliwahi kuifundsha Monaco kwa miaka 7 na kuiwezesha timu hiyo kuchukua vikombe vya ligi kuu ya Ufaransa,na UEFA CUP.Wenger aliikacha timu hiyo na kujiunga na washika bunduki wa London.
Arsenal itakuwa mara ya kwanza kutoka kwenye hatua ya 16 bora ya UEFA tangu mwaka 2010.
KIKOSI CHA ARSENAL.
Mfumi:4-4-2.
Ospina,Bellein,Mertasacker,Koscielny,Gibbs,Coquelin,Cazorla,Sanchez,Ozil,Welbek(chamberlain),Giroud.
Goli: Chamberlain 90+1 dakika.
KIKOSI CHA MONACO.
Mfumo:4-5-1.
Subasic,Toure,Wallace,Abde,Eldeson,Dirar,Kondogbia,Fabinho,Moutinho,Martial,Berbatov.
Goli. Kondogbia 38dk
Berbatov. 57dk
Else son. 90+4 dk
Mechi nyingne iliyochezwa jana ni Bayern Leverkusen 1 vs 0 Atletico Madrid.Gori la pekee hilo lilifungwa na Guilherme.
No comments:
Post a Comment