Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Wednesday, February 18, 2015

IZZO BIZNESS AELEZA KWANINI NGOMA YAKE NA SHAA "KIDAWA" NI TOFAUTI.

Rapper kutoka Green City Mbeya,Izzo Bizness,anatarajia kuachia ngoma yake ya kwanza kwa mwaka huu.Izzo amesema ngoma hiyo iitwayo "kidawa" itawagusa wengi na pia kubadili mahusiano mengi kimapenzi.

Akiongea na E- News ya EATV,Izzo alisema:-
Hii inakuwa rekodi ya kwanza mwangu kusimamiwa chorus na nyota wa kike ambaye ni shaa.Halafu unajua jina Kidawa ni majina ya watoto wa kike ambao wamezoeleka huko uswahilini.Huwezi kukuta mtoto anaitwa jina hilo Masaki,Mikocheni,Osterbay.Sasa humu nimemuelezea kuwa hili jina la kidawa unaweza kulinyambulisha tofauti na watu walivyozoea.Hii unaweza muelezea ata mtu wako wa karibu kupitia jina la Kidawa.Kwahiyo mashabiki wakae tayari kuskia ngoma hiyo"

Hivi karibuni kupitia Instagram,Izzo aliandika:
Naomba mnisikilize vzuri na naomba  mninukuu hii kauli yangu"Baada  ya video hii ya KIDAWA kutoka kwa asilimia 98% ya wanawake walioko kwenye mahusiano ( mapenzi ) watabadilika majina yao na kujiita wakina KIDAWA au a.k.a  zao zitakuwa KIDAWA...Fanya ya kumtag yoyote ambaye yupo kwenye mahusiano ajionee ili .KIDAWA VIDEO COMING SOON.

No comments:

Post a Comment