Msanii wa bongo fleva,Diamond Platnumz anauguliwa na mama yake mzazi kwa takrabani ya wiki sasa. Japo msanii huyo amekana taarifa hiyo kwa kusema maswala hayo ni yake binafsi.
Moja ya chanzo kinasema Mama yake Diamond ana wiki sasa yuko hospitali amelazwa na Diamond mwenyewe anaenda kumtembelea kwa kujificha ili watu wasijue.
"Mama yake Diamond,ana wiki sasa yuko hospitali amelezwa,Diamond mwenyewe anaenda kumuona wakati mwingne anaenda hadi saa 7 usiku,sijui anaficha nini? Ila tumuombee kwa mungu apone" kilisema chanzo hicho.
Diamond alipotafutwa alikataa kuliongelea swala hilo.
"Naomba unipe muda maana nina matatizo sana hata kuzungumzia ishu hiyo nadhani hakuna haja" alisema Diamond.