Upelelezi wa kesi ya kula njama ya kudhuru kwa sumu,inayomkabili Mkurugenzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Wilfred Lwakatare na mwenzake bado haujakamilika.
Wakili wa serial I Genes Tesha alidai hayo Jana mbele ya Hakim Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Janeth Kuluyenda wakati kesi hiyo ilipotajwa jana.
Hakimu Kuluyenda aliahirisha kesi hiyo hadi April mosi mwaka huu itajapotajwa tena kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi umekamilika.
Lwakatare na Ludovic Joseph wanadaiwa Desemba 28 mwaka juzi katika eneo la King'ong'o wilaya ya Kinondoni kwa pamoja walikula njama ya kutoa sumu kwa nia ya kumdhuru mhariri wa gazeti la Mwananchi Denis Mwacky.
Katika hatua nyingine upelelezi wa kesi ya mauajk ya kutokusudia kutokana na kuporomoka kwa jengo la ghorofa 16 inayiwakabili watu 12 bado haujakamilika.
Washitakiwa wa kesi hiyo ni Gabriel Fuime mfanyabiashara wa Laza Radha ,Diwani katika manispaa ya Kinondoni ,Ibrahim Mohammed (59), vigogo wa manispaa ya Ilala ambao ni mhandis Mkuu ,Charles 48, Mhandisi wa Majengio Godluck Sylvester (35) na mkurugenzi mkuu wa mkaguzi wa majengo,Willbrod Mugyabo (42)..
Inadaiwa machi 29 mwaka jana katika eneo LA India Gandhi Ilala ,Dar es Salaam bila kukusudia washitaliwa waliwaua watu 27.
No comments:
Post a Comment