Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Monday, March 2, 2015

TANESCO YAKIRI MADUDU KATIKA MFUMO WA LUKU.

Shirika la ugavi na usambazaji wa umeme nchini (TANESCO),limekiri kuwepo na matatizo ya mfumo wa kununua luku,ulioanza Ijumaa jioni wiki iliyopita hadi Jana na kuwa matatizo hayo yanatokana na mfumo wa kuuza umeme wa luku.

Akizungumza na mwandishi jijini Dar es Salaam Jana,Meneja wa Mawasiliano wa Tanesco ,Adrian Shogholo alisema ni kweli kuwa tatizo hilo lipo na limetokana na mfumo wa manunuzi wa umeme wa luku.

"Ni kweli tunaomba radhi wateja wetu kwamba kuanzia ijumaa jioni kilianza tatizo la kununua umeme wa luku kwa wateja wetu,ila tumegundua tatizo na mafundi wetu kwa kushirikiana na mafundi kutoka Afrika Kusini ambao walutengebeza mfumo huo,wanashughulikia tatizo hilo"alisema Shugholo.

Aidha aliahidi kwamba muda wowote kuanzia leo huduma zitaanza kupatikana na kwanba wakati tatizo hilo likiendekea kushughulikiwa  wateja wa luku wanaweza kununua umeme kupitia benki ya CRDB,NMB, na Max Malipo.

"Kuna wateja wanaotumia simu kunua umeme ,wapo waliotuma fedha na hawajarudishiwa majibu ya umeme,na wengine wamepata umeme  ila wakiingiza kwenye luku hauingii,wasihofu fedha zao ziko salama na watapata umeme tutawatumia mamba zingine ambazo wakiingiza zitakubali" alisisitiza Shogholo.

No comments:

Post a Comment