Msanii wa bongo Fleva Diamond Platnumz jumamosi iliyopita aliamia nyumbani kwake Tegeta Madale,baada ya mpenzi wake Zari kuhofia hali ya ushirikina ya Sinza Moli alipokuwa anakaa msanii huyo.
Chanzo kimeiambia Amani,kuwa Zari toka apate ujazito alipenda akae karibu na mpenzi huyo,ila kutokana na kuhofia hali ya ushirikina ya Sinza moli na kuhofia mimba yake kuweza kuchoropoka akashindwa kukaa nae. Awali Diamond alikataa kuhama Sinza kutokana na Tegeta ni mbali sana na misele yake ya siku.
"Ndugu yangu kama unataka kufahamu undani zaid ya huu ninachokueleza muulize Diamond mwenyewe atakwambia,Zari siku zote alikuwa anataka kuwa karibu na Diamond hasa baada ya ujauzito,lakini ndugu zake walikuwa wakiwakatalia kufanya hivyo hivyo kwa kuhofia mimba yake kuchoropoka kutokana na vijicho vya watu"
Jumamosi iliyopita Diamond alikata shauri na kuhamia kwenye makazi yake mwenyewe binafsi,baada ujenzi wa karibu miaka 3. Kwa mujibu wa mkandarasi mmoja, nyumba hiyo mpaka kukamilika imegharimu shilingi milioni mia nne (400 millions).
Credit:GPL
No comments:
Post a Comment