Mke wa rapper Noorah ,Camila amefariki dunia akiwa kwao Morogoro.
Akizingumza na WAKEREKETWA ,ndugu wa karibu wa marehemu ambaye hakutaka jina lake kutajwa amesema Camila baada ya kuanza kuugua alirudi nyumbani kwao mpaka mauti yalipomkuta hapo jana.
"Kweli amefariki alikuwa kwao Morogoro na bado haijajuliksna alikuwa anaumwa nini,na mume wake naye anaumea yupo kwao Shinyanga" alisema.
"Kwa hiyo msiba upo Morogoro ,kuna mtu ambaye anaelekea Morogoro sasa hivi akifika kule tutajua kila kitu. Moro alienda mda kidogo baada ya kuachana na mumewe. Baada ya kuachana Noorah alienda kwao Shinyanga na mke wake akaenda kwao. Hata hivyo hawakubahatika kuwa na mtoto," aliongezea.
Marehemu alikuwa anaitwa Anna Kigwali lakini baada ya kuolewa na Noorah alikuwa anaitwa Camila
No comments:
Post a Comment