Staa wa semina za kibongo asiye kaukiwa na matukio hapa nchini,Wema Sepetu aligeuka mbogo ghaflaa baada ya kupokea ujumbe uliomtaja mpenzi wake was zamani (Diamond) kutoka kwa shabiki yake.
Kioja hicho alikifanya juzi nyumbani kwake,Kijitonyama Dar es Salaamvalipokuwa akirekodi kipindi chake chake cha In My Shoes ndipo aliposhituka baada ya kutumiwa maoni na mmoja wa mashabiki wake kupitia simu ya mkononi.
"Heee huyu vipi tena ananitajia jina hili (Diamond),sitaki kabisa kusikia,hapa nataka kusikia mimi na maisha yangu na si maisha ya mtu mwingine." Alisikika akisema Wema.
No comments:
Post a Comment