Rich Mavoko amesainishwa na kampuni ya usimamizi ya Kenya iitwayo Kaka Empire iliyoanzishwa na Rapper Rabbit.
Kampuni hiyo inawasimamia wasanii wengine kazi zao ambao ni Avril,Raj,Femione name Owanjo.
Mavoko ameiambia Bongo 5 kuwa kampuni hiyo itakuwa inasimamia kazi zake zote kwa upande wa Kenya. Pia ameeleza sababu ya kufanya uamuzi wa kusaini na kampuni hiyi ni kuwa amegundua ana mashabiki wemgi Kenya na kuna watu wanafaidika kwa kuuza kazi zake.
"Nimekuta midundo.com kuna anachukua hela zangu tangu miaka 3 nyuma,tangu nyimbo ya mbona ,so hela ndogo ni dola kadhaa. Yule jamaa alienda kujitambulisha kama meneja wangu"
"Kwahiyo jamaa wakaniambia kuwa haukuwa na mtu anayeweza kufuatilia vitu vyako vya Kenya kwahiyo inabidi upate wakala au mtu wa kusimamia kazi zangu za Kenya naye atakuwa anachukua asilimia kadhaa ila haki zako zote nitazipata" aliongeza Mavoko
No comments:
Post a Comment