Nay wa Mitego majuzi kupitia akaunti yake ya Intagram aliweka wazi majibu yake ya UKIMWI kuwa hakuwa muathirika .
Leo hii katika mahojiano Nay wa Mitego amefunguka Kuwa alipima ngoma kwani alikuwa anaumwa Malaria ndipo alipo amua na kupima ukimwi.
"Nilipima baada ya kuwa na malaria lakini huwa ni kawaida yangu kupima ngoma,hata mke wangu (Siwema) alipokuwa mjamzito tulienda pammoja kupima hospitali,"alisema Nay
Alipoulizwa tangu alipoanza mahusiano na mke wake Siwema allishawahi kuchepuka,alikiri ni kweli ila hawezi kusema mara ngapi ili kuinusuru ndoa yake.
"Unajua ni mambo ya ujana, ni kweli nilishawahi kuchepuka lakini siwezi kusema mara ngapi si unajua mama watoto anaweza kukasirika? Lakini nilikuwa makini sana na nina muomba sana msamaha mke na sitegemei kuchepuka tena,"alisema Nay.
No comments:
Post a Comment