Katika maisha unaweza ukafanikiwa kupata rafiki wa dhati si mnafki,na rafiki wa dhati mnafki. Unaweza ukamuamini rafiki yako kwa kila jambo kumbe yeye anatumia hiyo nafasi kukumaliza. Ndivyo ilivyotokea kwa marafiki vipenzi wa tasnia ya filamu nchini Wema Sepetu na Kajala Masanja,baada ya Kajala kumsaliti rafiki yake huyo aliyemtoa jela kwa mmoja wa mpenzi wa Wema.
"Nimetumia ujanja wa hali ya juu hadi nikafanikiwa kuzipata SMS za Kajala na yule kigogo wa Wema,kama vipi niwatumie"kilisema chanzo chetu.
Kama hiyo haitoshi chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa SMS hizo zilionesha namna Kajala alivyokuwa wakiitana baby na kigogo huyo,huku wakiwa kwenye mahaba nizamishe,kiasi cha kigogo huyo kuwagharamia wazazi wa Kajala.
"Jamaa walikuwa wanapika na kupakuwa kigogo alikuwa akigharamikia kila kitu kuanzia misosi ya nyumbani,usafiri wa location na hat a kwa wazazi wa Kajala alikuwa anatuma Fedha " chanzo hicho kiliendelea kutiririka.
Mwanahabari wa GPL alifanikiwa kuzipata SMS hizo na kujionea majibizano ya muda mrefu huku zikitaja marafiki wa karibu wa Kajala anaofanya nao kazi kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment