Mrembo na staa wa Bongo muvi Jacqueline Massawe Wolper amefunguka kuwa anaijua thamani yake kama msanii hivyo hawezi tumika na wafanyabiashara kwa kutangaza biashara zao bila kuwa na mikataba inayoeleweka au mtu kumfanyia maamuzi pasipo kuwa na makubaliano na kufika mwafaka kuhusu hilo.
"Kujenga jina katika sanaa si kazi ndogo unapigana kujitoa na inapotokea kuwa maarufu watu wanaanza kuona thamani ya Jina lako ulilojijengea basi ni wakati wa kulipia na si bure tena," alisema.
Jacqueline hivi karibuni alikataa kupiga picha na kampuni moja baada ya kutaka apige picha akiwa ameshika bidhaa yao huku wakimlaghai Kuwait wateleta zawadi. Pia picha ya bidhaa hiyo aweke kwenye akaunti zake za kijamii kwa kuwa ana wafuasi wengi.
No comments:
Post a Comment