Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Popular Posts

Search This Blog

Popular Posts

Popular Posts

Tuesday, March 10, 2015

DULLY SYKES: MIMI NI KAMA BONDIA NISIYEPIGWA KWA KO.

Dully Sykes amejitapa kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii wasioyumbishwa na hali ya mziki kutokana na ubishi alionao kwenye game na aina ya muziki anaofanya.

Dully ambaye anatarajia kutoa video ya wimbo wake "Shuka" ameiambia Bongo5 kuwa yeye tayari anaujua mziki vizuri na hivyo si rahisi kuteteleka.

"Baada ya kumaliza matatizo narudi rasmi na video ya wimbo Shuka ambayo nimefanya na Adam Juma,mimi kwenye muziki ni kama boxer ambaye hata nikipigwa siwezi nikapigwa KO. Mimi ni boxer mzuri sana hata Rashid Matumla alishapigana na Cheka lakini Cheka alimpiga Matumla lakini siyo kwa KO,alihangaika sana kumpiga na mimi ni bondia ambaye nikifanya mazoezi nampiga hata bingwa wa uzito wa juu," amejitapa msanii huyo.

"Kwa hiyo mimi siogopi kubadilisha muziki wangu kisa mtu fulani amefanya kitu fulani. Mimi ni mtu ambaye nafanya muziki wangu na unajulikana kama muziki wa dully Sykes ni muziki wa uhakika,"

No comments:

Post a Comment