BUNGE limpetisha rasmi muswada wa sheria ya udhibiti wa madawa ya kulevya kwa mwaka 2014,huku adhabu ya kifo watakaotwa na tuhuma ya biashara hiyo ikitupiliwa mbali. Na kufanya adhabu ya Faini ya shilling billion moja au kifungo cha miaka 30 jera kama njia ya kudhibiti biashara hiyo haramu.
Baadhi ya wabunge wanaendelea kung'ang'ania adhabu ya kifo iwekwe kwenye muswada huo.
Akitoa majumuisho ya michango ya wabunge kuhusu hoja ya muswada huo,Waziri wa Nchi,ofisi ya waziri mkuu,Sera,uratibu na bunge Jenista Mhagama alisema adhabu ya kifo haiwezekani kuwekwa kwenye sheria kwa sababu ina makosa mawili.
"Ni kweli Tanzania ni miongoni mwa nchi ambayo bado zinatoa adhabu ya kifo ,lakini kwa mujibu wa Sheria iliyopo,adhabu ya kifo imeingizwa na kubainisha kwenye makosa ya mauaji." Jenista Mhagama.
Je ni kweli adhabu ya faini ya billion 1 au kifungo cha miaka 30 jera itaweza kudhibiti biashara hiyo nchini? Maana mfanya biashara wa madawa ya kulevya kwa mwaka anaingiza zaidi ya mabilion ya pesa.
No comments:
Post a Comment