Mamlaka ya udhibitu usafiri wa nchi kavu na maji (SUMATRA) imeanza mchakato wa mapitio ya viwango vya nauli ya mabasi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya mkurugenzi mkuu wa SUMATRA ,mapitio hayo yana lengo la kubaini haja ya kurekebisha viwango vya nauli za mabasi nchini.
"Kwa mujibu wa sheria za SUMATRA ya 2001 na kanuni zake,mamlaka imeamua kufanya mapitio ya viwangi vya juu ya nauli nchini kwa lengo la kubaini haja ya kufanya marekebisho. Ili kutimiza hili mamlaka inatakiwa kukusamya maoni ya wadau kabla ya kufanya maamuzi wa kuridhia viwango vya tozo kwa huduma zinazothibitishwa na mamlaka zikiwemo nauli za mabasi," alisema.
SUMATRA imeaandaa mikutano ya kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali,wakiwemo watoaji wa huduma hiyo na wananchi kwa ujumla.
Taarifa hiyo inaonesha ratiba ya mikutano ambapo mkutano wa kwanza umepanga kufanyika jumatatu ijayo katika ukumbi wa Gold Crest Hotel,utafatiwa na mkutano wa machi12 utakaofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Kigoma na watatu utafanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi was Karimjee machi 18.
Akizungumza hilo katibu mkuu wa Chama cha kutetea Abiria (CHUKUA),GODWIN NTOGEJI alisema waliandikia barua SUMATRA waweze kushusha nauli ya mabasi ili wananchi waweze kunufaika kwa kushuka bei ya mafuta nchini.
"Awali tuliwaandikia barua SUMATRA hawakujibu,baada ya muda tukawandikia barua ya kuwakumbusha na ndipo walipotujibu na tunashukuru tumeshaona matangazo ya kuwaita wadau kujadili nauli."
No comments:
Post a Comment