Mwanasheria mkuu wa CHADEMA,Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa uwanachama wa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali pingamizi la mbunge huyo kuzuia asijadiliwe.
"Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA,mwanachama anapufungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake,na endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejitoa uanachama wake ,kwa hiyo natangaza rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa CHADEMA"
Kwa upande wake Zitto Kabwe amesema hakuwa na wito wa mahakamani leo,na jaji wa kesi kahamishwa Tabora na hakuna taarifa ya jaji mpya,pia kaongeza kuwa mwanasheria anafuatilia na atatoa statement.
No comments:
Post a Comment